SWALI :COMPUTER YANGU IMEBADILISHIWA WINDOW NA KUWEKA WINDOW 7 LAKINI SIPATI SAUTI.
TATIZO NINI?
JIBU:POLE KWA USUMBUFU HUO,
TATIZO LA HIVYO LINAWEZA SABABISHWA NA VITU VINGI SANA SIO KAMA UNVYOWEZA FIKIRIA
1.ANGALIA DRIVER ZA SAUTI NDANI YA COMPUTER YAKO KAMA ZIMEINGIA KWA KUFUATA NJIA IFUATAYO,
i- right click my computer- properties then fuata njia zifuatazo kama invyoonekana katika picha
hapo utaingia upande wa device manager kisha utakwenda kuangalia multmedia and audio kama utakuta hakuna alama ya njano katika eneo hilo elewa kwamba computer yako ipo safi upande wa driver na ukikuta kuna alama ya njano elewa kuwa hilo ni tatizo na fanya utaratibu wa kutafuta hiyo driver au ukishindwa nenda kamuone mtaalamu akusaidie.
2.ni lazima ujue ya kwamba hiyo computer uliyopokea imetengenezwa kwa default ipi kwanza kupitia uzoefu wangu nitakueleza kitu "wengi wetu tumekuwa tukipenda kutumia window 7 kama operating system ambayo ni mpya" sio kila computer ukiweka window 7 basi utapata kile unachokihitaji kutoka katika window 7 na moja ya tatizo ni kukosekana kwa sauti hapo unatakiwa kujua kuwa hiyo sio chaguo sahihi la computer yako.
3.badala ya kufanya test za software lakini bado kujapata jibu sahihi au suluhu ya tatizo lako basi ndio wakati mwafaka wa kufikiria katika vifaa yani HARDWARE.
hapo kuna ishu tena na majibu ya hapa ndio yatakayo amua jibu moja kama computer yako imeharibika njia ya sauti au lah.
I.muulize mteja wako kama anatumia earphone au speaker za nje kusikilizia katika computer yake jibu likiwa ndio basi,tembelea eneo la hapo ndani ya computer then check kwa umakini sana maana huwa kuna pini inayo gusa sehemu ya bodi ya computer pindi unapochomeka stereo pini sasa ukichomoa vibaya itagusa bodi yako na kamwe hautapa sauti mpaka urekebishe huo mfumo.vinginevyo unaweza fikiria juu ya hardware kuharibika.